Kwanza nitoe pole kwa watanzania wote walioguswa kwa vifo vya watu wawili vilivyotokea Mtwara wa sababu ya mgogoro wa serikali na wananchi juu ya rasilimali ya gesi. Nafsi yangu imesikitishwa kwa masaibu yaliyowapata ndugu zangu, watanzania wenzangu huko katika ardhi ya Mtwara nchini Tanzania. Mungu awafariji wale wote waliwapoteza ndugu zao. Ninajua hali ngumu mliyonayo kwa sasa kwa kufiwa na ndugu zenu wapendwa. Mungu awapumzishe wale waliofariki.
Pamoja na hayo yote lakini nafsi yangu inazidi kuumia kila siku ninapotafakari yaliyotokea nchini ikiwa ni pamoja na hili la Mtwara. Mengi yamesemwa na mengi yameandikwa lakini pia nina machache ya kuandika hapa. Nimejaribu kujizuia lakini naona machozi ya nafsi yangu yanazidi na kunishinda kuvumilia. NIlikwiahawahi kuandika juu ya utajiri mkubwa wa nchi yetu ambao unatosha kabisa kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa makubwa kiuchumi Duniani. Ila ni ukweli usiopingika kuwa wapo watanzania wanaofanya vyama vyao kama mtaji wa kula nchi peke yao.
Kwa ufupi nieleze utajiri wa nchi hii yetu inayotamaniwa na mataifa mengi si tu kwa ajili ya amani kama wengi wanavyosema bali inatamaniwa kwa sababu ya utajiri wake wa maliasili uliokithiri. Na sasa tunaanza kupatwa na taabu, mateso, majonzi na simanzi kwa sababu ya utajiri wetu badala ya kufurahi huku tukimtukuza Mungu kwa kutupendelea watanzania. Naumia kuona utajiri wetu wa maliasili unaanza kugeuka balaa badala ya kuwa baraka.
Baada ya serikali kuwa na kuendelea na mpango wake wa kujenga bomba la gesi ili kusafirisha gesi hiyo kutoka mji wa Mtwara hadi Dar es Salaam, wananchi wa Mtwara wamekuwa wakihoji watanufaika namna gani na mradi huo. Baada ya serikali kupitia waziri wa nishati na madini Mh. Prof. Muhongo kusisitiza kuwa mpango huo wa kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi jiji lenye msongamano wa watu kuliko majiji yote hapa Tanzania upo pale pale, wananchi wa Mtwara nadiriki kusema walikereka, iliwauma na kuamua kuonesha hisia zao kwa serikali yao waliyoichagua wenyewe na kwa watanzania wote kwa ujumla kwa kuamua. Maandamo yao ni ishara tosha kuwa wanamtwara hawakuridhika na mpango huo. Binafsi inanipa taswira kuwa hakukuwa na maelewano kati ya serikali na wanchi wa Mtwara.
Mara kadhaa viongozi waandamizi wa serikali ya Tanzania wamesisitiza kuwa wananchi wa Mtwara waelimishwe. Kauli kama hii ina maana gani? Je inamaana wananchi wote wa Mtwara hawana elimu, hawalewi au hawajui umuhimu na manufaa ya kuwa na gesi? Kama hivyo ndivyo, hivi nani wa kulaumiwa wana-mtwara au serikali iliyowaacha wanamtwara kwa miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru bila kuwapatia elimu stahiki? Je kutokuwa na elimu kwa wanamtwara kunakuja tu baada ya kupatikana gesi?
Haya ni maswali madogo na mepesi tu yeyote anaweza kujiuliza. Lakini kwanza hebu tuljiulize juu ya rasilimali tulizonazo. Nimegundua si wanamtwara peke yao ila hata mimi nahitaji kuelimishwa au kupewa ufafanuzi au majibu ya mawasli mengi niliyonayo na pengine waliyonayo wanamtwara na watanzania kwa ujumla.
Kwanza baada ya kuonekana gesi imegundulika nataka kujua ni gesi kiasi gani iliyopo au inayokadiriwa kuwapo? Je inakadiriwa gesi hiyo inweza kwisha baada ya muda gani? Je tutegemee taifa letu kuwa na gesi kwa miaka mingapi ijayo? Lakini pia kwa mujibu wa jiografia yangu ya darasa la sita enzi hizo je hii gesi haiambatani na uwepo wa mafuta?
Sote tunafahamu kuwa jiji la Dar es Salaam linamsongamano mkubwa wa watu na magari. Jiji la Dar es Salaam lina viwanda vingi ambavyo vinaendelea kufanya kazi. Mtu akipata ajali inakuwa ni dharura na hivyo ni lazima awahishwe hospitali na mara nyingi kunakuwa hakuna muda wa kusubiri. Hii gesi imegundulika kama dharura? Kwa maana kwamba ni lazima tuichimbe gesi haraka haraka na kuisafirisha maana itapotea.
Lakini kwa suala la nchi kuwa na gesi ambayo hata watanzania hawajaambiwa ni nyingi kiasi gani, na faida itakayopatika itaitoa nchi kutoka hali gani hadi kufikia hali ipi ya kimaendeleo na hali hiyo itazamiwa kufikiwa baada ya muda gani? Je gesi haiwezi kusubiri mazungumzo na makubaliano au elimu kwa wananchi? Na kama serikali inadhani kwa kujenga bomba la gesi ndiyo inaharakisha maendeleo mbona almasi tunayo na hali ya kiuchumi ya watanzania bado inazidi kuwa ngumu? Mbona dhahabu tunayo? Mbona tuna tanzanite madini ya thamani yasiyopatikana Duniani kote isipokuwa Tanzania na bado watanzania wengi wanavaa pete za mabati? Mbona maziwa na mabwawa mazuri tunayo na bado tunalia njaa nchini na hata minofu ya samaki hailiwi na mtoto wa kijiji cha mlimani kata ya Lupembe-Mtwara? Mbona tunayo makaa ya mawe yenye ubora kuliko hata makaa ya mawe yanayopatikana Afrika ya Kusini na bado tunamgao wa umeme? Mbona tuna chuma lakini bei ya nondo au vifaa vya ujenzi inazidi kupaa? Mbona tuna mbuga za wanyama, misitu na milima yenye kuingiza fedha nyingi za kigeni na bado watanzani wanahesabika kuwa miongoni mwa watu masikini duniani? Hivi mbona Mtwara kuna korosho zenye ubora kuliko zote duniani na bado hali ya maisha ni ngumu?
Kikubwa zaidi ambacho kwa kweli kimenisononesha hakuna uvamizi kutoka nchi nyingine bali ni sisi kwa sisi tunavurugana na hata kusababisha kupoteza uhai wa wananchi wasio na hatia. Binafsi bado sielewi, ninahitaji majibu.
Ni kitu gani ambacho hakipo Mtwara na kwa kweli hakiwezekani kamwe kujenga Mtwara? Eneo la bahari ya Mtwara ni zuri kwa ujenzi wa bandari. Na uzuri wake ni zaidi ya eneo la bandari ya Afrika Kusini. Wakenya wanapanua bandari ya Mombasa hadi kufikia gati 22, sisi tunataka kuanza kuchimba bagamoyo badala ya kujenga ya Mtwara na kupanua za Dar es Salaam na Tanga. Je, gesi hii ambayo binafsi ninaiona kama nyongeza muhimu katika taifa na fursa nzuri kwa nchi yetu kwamba baada ya kutojikwamua kutoka katika umasikini licha ya kuwa na madini, mito, maziwa, bahari, milima, misitu, wanyama pori na kila utajiri wa nchi hii basi angalau kwa gesi tungejipanga. Nilitegemea baada ya sekta ya madini kulalamikiwa, sekta ya kilimo hivyo hivyo basi kwa gesi serikali ingejaribu kwa kila hali kuhakikisha si tu watanzania wanavuka bahari ya umasikini bali wanafarijika na kuridhika na mipango mikakati na utekelezaji wa mipango hiyo katika uchakataji, uvunaji na utumiaji wa gesi. Kwa nini gesi ipoteze uhai wa binaadamu? Uhai ambao haupatikani sehemu nyingine yoyote.
Hivi kweli serikali haipendi mikoa ya Lindi na Mtwara na Tanzania kwa ujumba kuwa miji, kuwa na viwanda na biashara angalau kama Dar es Salaam? Nikiwaza zaidi najiuliza hivi Mtwara si Tanzania? Gesi ikipelekwa Dar es Salaam inakuwa kwa manufaa ya watanzania wote, je ina maana miundo mbinu inayohitajika ikijengwa Mtwara na kusafirisha mazao ya gesi na kiasi cha gesi kinachohitajika kwenda sio tu Dar es Salaam ila kwenda nchi nzima inakuwa si kwa manufaa ya watanzania wote? Ukisema ukweli inaonekana eti ni uchochezi. Nitasema ukweli daima maana sio tu kwamba uongo ni dhambi lakini pia wazazi wangu walinifundisha kusema kweli kwa gharama yoyote. Hivi kwa nini Dar es Salaam tu? Kama lengo ni ili gesi iwanufaishe watanzania au ionekane ni kwa manufaa ya watanzania kwa nini hawaipeleki mkoa wa Dodoma, ambapo ni makao makuu ya nchi yetu?
Hoja hizi zinazotolewa na viongozi wetu binafsi zinanipa shida na zaidi sana nadiriki kusema zinadhalilisha weledi? Kuna kauli zinadhalilisha wasomi wazalendo wa nchi hii. Hivi kiongozi anaposema hakuna gesi bila mabomba anataka tumueleweje? Tukimjibu kwa majibu mepesi yanayolingana na hoja yake kwa kusema, sawa basi bomba lianzie Mtwara mjini na liishie Masasi tutakuwa tumekosea?
Kiongozi mkubwa unaposema wana-Mtwara hawataki kushea gesi na watanzania wengine, hivi tangu lini wananchi wa Mtwara wana mitambo ya kuchimba gesi? Hawa wanamtwara ninaowafahamu mimi tangu lini wakawa na ubinafsi wa aina hiyo huku korosho zao zikiuzwa ulaya kwa bei ya juu kupindukia? Hawa wanamtwara eti wawanyime wataanzania gesi lakini wanaachia korosho zao huku wakilia njaa? Nadhani ifike mahali ukweli usemwe wazi bila kuangalia anayeambiwa ni nani.
Baba wa taifa hayati Mwl. Julius Nyerere mbona alijega viwanda vingi katika maeneo kunakopatikana mali ghafi husika? Au ina maana alikuwa hana akili? Viwanda vya nguo vijengwe mahali pamba zinakolimwa kwa wingi. Viwanda vya katani vijengwe kunakolimwa katani kwa wingi. Viwanda vya samaki vijengwe kunakozalishwa samaki. Na hatujawahi kusikia mtanzania hata mmoja akilalamika eti kwa nini kiwanda cha mkonge kijengwe Tanga na siyo Simanjiro. Sijawahi kusikia mtanzania akilalamika kiwanda cha ngozi kujengwa Musoma. Hakika sijawahi kusikia mtazanania akilalamika na kutaka kiwanda cha kubangua korosho kijengwe Mwanza.
Nifikiria zaidi mawazo mengine ya ajabu yanakuja kichwani mwangu. Naanza kufikiri au kuna kitu nyuma ya pazia? Hivi ujio wa rais wa China na mikataba hiyo 17 inahusu nini? Nilimsikia waziri wa nishati na madini nchini Prof. Muhongo akisema mikataba sio siri kwa hiyo mtanzania anayetaka kuiona aende ofisini kwake apate nakala. Nimejiuliza sana nikaona nisiseme mengi, pengine kweli alisema kwa nia njema. Lakini nadhani kwa kuwa sio siri na ameruhusu kwa mtu yeyote kwenda kuchukua basi kurahisha kazi, nashauri kila Mbuge akachukue nakala na kuwaelezea wananchi kilichomo kwenye mikataba hiyo. Hivi kweli hata robo ya wananchi wa Tanzania ambao ni zaidi ya milioni 10, wakidai kupatiwa hizo nakala za mikataba wizara ya nishati na madini itaweza kutoa nakala hizo kwa watu wote hao? Au ni siasa tu?
Nisiseme juu ya ujio wa rais wa Marekani na ujumbe wake wa watu 700. Laini kila mtanzania ana haki ya kujiuliza haya mataifa makubwa kweli wanatupenda watanzania? Tupime kati ya amani yetu na maliasili zetu ipi wanakitamani?
Tuache siasa uchwara tutoe hoja zenye maslahi kwa Taifa. Serikali iseme kwa nini inaharaka na kusafirisha gesi badala ya kuwa na haraka ya kuhakikisha watanzania wanapata maelezo ya kutosha juu ya gesi. Serikali iseme, ni faida zipi zitapatikana mradi ukianza kwa gesi kwenda Dar es Salaam kabla ya kujenga miundombinu ya kutosha katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Serikali ituambie hasara itakayopatikana kwa kuanza na ujenzi miundo mbinu Mtwara na baadaye kuendelea na mipango ya kusambaza gesi hiyo katika mikoa mingine kulingana na uhitaji wa mkoa husika. Serikali iseme kama Mwanza, Arusha na Mbeya hawahitaji gesi mapema ukilinganisha na Dar es Salaam. Serikali iweke bayana kwamba ni lini itasambaza gesi mikoa yote nchini na kwa nini ianze Dar es Salaam na si Mtwara, Lindi Ruvuma, Dodoma n.k. Serikali haina budi kutamka wazi bila kumumunya maneno kama wanamtwara hawana haki ya kujua wananufaika vipi. Iseme kama ina uhakika kwamba wanamtwara na watanzania wameelewa sawia juu ya mpango wake wa kuanza kwa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam. Na kama bado wananchi hawajaelewa kwa nini itumie nguvu badala ya meza ya mazungumzo kuwaelewesha wapiga kura wao? Gesi ni kwa jili ya wananchi si kwa ajili ya watawala. Gesi itumike wapendevyo wananchi kwa kuwa na mipango ya kitaalamu na si kisisasa.
Kwanini tufe hali gesi ni yetu, serikali ni yetu, Mtwara ni yetu na Tanzania ni yetu?
Mungu isaidie Tanzania Mungu isaidie Afrika.
George Adriano

0 comments:
Post a Comment