SERENGETI

Serengeti, The Proud Of Africa.

LEADERSHIP

We Need Leaders: Nelson Rolihlahla Mandela, The Icon Of Africa.

BOOKS

The Powerful Book! Written by Young African Author; Dr. George Adriano.

BUNGE LETU

BUNGE LIWE DARASA KWA WATANZANIA

GREATNESS

Develop Yourself and Become Great. Dr. George Adriano

Showing posts with label LEADERSHIP. Show all posts
Showing posts with label LEADERSHIP. Show all posts

Monday, March 24, 2014

WATANZANIA WANAHITAJI DIKTETA?

Udikteta ni mfumo wa kiutawala ambao mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu huwa na mamlaka yote katika nchi au Taifa ambayo mara nyingi huyapata, kwa kutumia nguvu. Ikiwa amepata madaraka kwa njia ya demokrasia ili awe dikteta ni lazima endeshe nchi kinyume na misingi ya demokrasia. Kwa hiyo dikteta hafuati kanuni za kidemokrasia na wala si lazima afuate sheria halali za nchi.

Kiongozi dikteta si lazima apendwe na watu. Si lazima atekeleze sera mlizojiwekea. Dikteta anaweza kufanya au kuwafanyia lolote ambalo anaona linafaa, kwa manufaa yake au na watu wake wachache. 

Wapo baadhi ya watanzania wametamka, wengine kwa siri na wengine wametamka wazi kabisa kuwa ni vema wawe na Rais dikteta. Wanataka Rais dikteta. Haina maana hawapendi amani na utulivu ila hoja ni kwamba wamechoshwa na mafisadi, na wizi wa mali za umma na kutokuwajibika. Kwa hiyo wanataka Rais dikteta atakayepambana na mafisadi katika nchi. Wanahitaji dikteta wa kupambana na rushwa katika Taifa. 

Baadhi ya watanzania wanahitaji dikteta atakayewatia watu adabu ili waondokane na uvivu; ili watu wawe wawajibikaji na hatimaye kujenga Taifa lao. Hawataki Taifa lenye watu legelege.

Dhana hii imejitokeza baada ya kuibuka na kuibuliwa kwa vitendo lukuki vya kifisadi, rushwa na mikataba mibovu yenye kila harufu na rangi ya rushwa, na haya yakifanywa na watu waliopewa dhamana ya kuiongoza nchi, yaani viongozi.

Rushwa zimetajwa kwa baadhi ya mawaziri na wengine kufikia hatua ya kujiuzulu nyadhifa zao. Rushwa kwa viongozi waandamizi wa serikali katika wizara mbalimbali na hata mashirika na taasisi za umma. Wapo waliofikishwa mahakamani.Wapo waliokutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na wakaadhibiwa kwa kifungo na wapo walioonekana kutokuwa na hatia kisheria na kuachwa huru. 

Dhana ya kuhitaji dikteta ni dhana iliyokuja katika mawazo ya baadhi ya watanzania baada ya kuona kana kwamba hakuna suluhu juu ya mwelekeo wa nchi. Wananchi wengi wanaona kuwa wao hawana nguvu wala uwezo wa kuwashughulikia viongozi au watawala wao hasa wale walio wabovu. 

Wasomaji wangu hizi ni sehemu ndogo za ninachokiandika.... nahitaji maoni yenu.
George Adriano

Wednesday, March 12, 2014

WELCOME TO AFRICAN LIVES! FOR YOUR PERSONAL DEVELOPMENT