Monday, December 31, 2012

MWAKA 2013 UWE WA FURAHA KWAKO

Mpendwa, Heri ya Mwaka Mpya 2013!
Shalom!

Ikiwa kuna kitu chochote ambacho hakikukufurahisha au kilikuumiza au ulikosea na kushindwa kufikia malengo au matarajio yako, achana nacho. Acha kila lisilo jema libaki 2012.  Wewe fungua ukurasa mpya wa mwaka huu 2013. Anza yote ukihesabu kuwa kila baya limekwisha kama ulivyokwisha mwaka 2012.

Mungu amekupa nafasi nyinge ya kuanza upya pale uliposhindwa na kurejea pala ulipokatia tamaa na kusonga mbele. Futa kumbukumbu ya mabaya yaliyopita.

mungu awe mlinzi wa maisha yako na familia yako, jamaa zako, marafiki na wote unaohusiana nao. Mungu awe kiongozi katika kila ufanyalo. Baraka zikaonekane kwako. Kila anayekutazama wewe amuone Mungu, na kila anayekusifu wewe sifa ziende kwa muumba wa mbingu na nchi.

Usikate tamaa, endelea mbele nuru ya mbinguni itakuangazia nawe hutapotea kamwe. Uzima wa milele ububujike ndani yako, tangu sasa na hata milele,
Amina


Dk George Adriano

0 comments:

Post a Comment