Thursday, February 14, 2013

Nakutakia Valentine Yenye Furaha


Siku kama ya leo ni siku ya kutakiana Happy Valentine kwa kupeanza zawadi na maua kuonesha upendo kwa wale uwapendao. Kwa hiyo kila mmoja hasa wale wanaofuatilia maanani na kufuatilia siku hii ya leo basi huwa na maana kubwa sana kwao.
 
Leo mimi nataka kueleza machache hasa kwa wale ambao inawezekana kwa namna moja au nyingine hawana furaha saaana. Najua wapo wengi tu ambao umewatakia na kuwaonesha upendo wako siku ya leo ikiwemo wazazi, ndugu, jamaa na hata marafiki. Lakini furaha yako inakuwa imefifia kwa sababu ya kuumizwa na yuleee, aliyekuwa rafiki yako au mchumba aliyekuacha.

Inawezekana unamkumbuka kila mara na inakupa shida. Rejea somo langu lililosema "Sometime you have to be alone, Yes!" . Ndio, kuna wakati unatakiwa kuwa peke yako. Ukipitia kipindi kama hicho usipopoteza utu wako, hakika unakuwa bora zaidi kuliko hapo mwanzo. Ni wakati wa kujifunza na kuona thamani yako hata unapoachwa na unapokwa peke yako.

Lakini pia inawezekana upo na rafiki au mchumba wako kwa sasa. Pamoja na kuwa upo naye huyu ila ukweli ni kwamba yupo yuleeee uliyekuwa naye hapo mwanzo. Na sasa unamkumbuka sana na wakati mwingine inakupa shida kidogo. Hasa pale unapokumbuka baadhi ya matukio ambayo mlikuwa pamoja. Mbaya zaidi ni kama ulimvulia nguo hasa kwa wadada. Japo si nzuri hata kwa wakaka pia.

Pole, najua nimekukumbusha machungu lakini nia yangu si kukuumiza ila ni kukutoa kutoka hatua moja na kukusogeza hatua nyingine iliyo bora zaidi. Sikiliza, hakuna aliye mkamilifu, pamoja na yoooote uliyofanya ambayo hata nafsi yako inaona kabisa si sahihi lakini tambua kuwa wewe si wa kwanza kukosea, vilevile haina maana kuwa ndio baaaasi kwa kufanya kivyo eti haufai, la hasha. Wewe ni wa thamani ikiwa utatambua hilo na kuwa wa tofauti.

Mambo yaliyopita yanaweza kukuumiza ikiwa hayajapona, lakini ukielewa ninachotaka kukufundisha leo, kamwe hayatakuwa kidonda ila yanaweza kubaki makovu. Tofauti ni kwamba kidonda kinauma ila kovu mara nyingi haliumi ila linakufanya kuwa makini zaidi.

Napenda kusema hakuna kitu kizuri mtu unapotambua kwamba ulikosea, na ukaamua kuwa makini. Usiwe mwoga hata kidogo. Hakuna haja ya kuogopa eti kwa sababu ya yule aliyepita au wale walipoita walikusaliti. Hakuna haja ya kuwachukia wengine eti kwa sababu ya mabaya ya fulani. Duniani watu hatufanani hata kidogo. Kila mtu ana sifa zake, mapungufu yake na uzuri wake pia. Vinaweza kulandana kwa sehemu lakini si kwa asilimia mia moja.

Jambo la msingi tambua kuwa huna alama au bango linaloonesha mambo yako yaliyopita kila unapotembea. Kwa hiyo huna sababu ya kuendelea na makosa eti kwa sababu ulikosea ila ni wakati sawia wa kuanza upya. Kurekebisha makosa, kujenga utu wako wa ndani automatically utu wa nje utakuwa sawa. Binafsi huwa namwamini aliyewahi kukosea halafu akaelewa kuwa alikosea na kuambua kubadilika japo nawaamini ambao hawajakosea pia. Mara nyingi huwa wanakuwa makini, imara na hawakurupuki, tena hawaendeshwi na hisia tu bali hupima mambo kabla ya kuchukua hatua.

Epuka kufanya maamzui ya kudumu kwa vitu vya kupita. Achana na yaliopita kwa maana ya kukusumbua ila yatumie kama shule au guides za namna ya kufanya ya sasa na yajayo.

Namna Ya Kumsahau Aliyekusaliti

Unajua inawezekana kabisa ukawa na rafiki, mchumba na wakati mwingine hata mume au mke lakini bado ukimkumbuka yule aliyekuacha unaumia. Yaani unatamani uwe naye. Wakati mwingine unakumbuka mlipokuwa pamoja. Maeneo mliyokuwa mnapendelea kwenda n.k Hii inaweza kuwa hatari kwa uhusiano wako mzuri wa sasa. Hasa ikiwa uliingia katika uhusiano huu kwa umakini na sio eti ili umkomoe aliyekuacha kwamba akuone upo na mwingine. Yaani hukukurupuka, haukuwa desparate na haukuwa emotional.

Mtazamo huu niliupata jana tu, nilipokuwa natafakari juu ya kijana mmoja ambaye yeye alikuwa na rafiki yake na walipanga kuoana. Huyo mwenzake hakuwa mwaminifu. Kwa vijana wa leo niseme ni kama alikuwa anamzuga tu au ndiyo tabia yake. Baada ya huyu kijana kugundua hilo, aliumia sana. Sasa mwenzake alipoona kuwa siri zake zimekuwa wazi akaamua kumuacha- akampiga kibuti. Kwa hiyo huyu kijana akawa anaumia hasa anapokumbuka good moments walipokuwa pamoja. Si unajua alimpenda, kama ulivyofanya wewe pengine.

Ghafla nikapata hii revelation na ninaamini ikiwa kweli unampenda au mnapendana na rafiki, mchumba au huyu mwenzi wako wa sasa, basi itakuwa ni nafasi nzuri ya kusahau na kumsahau yule aliyepita, mliyeachana naye.

1. Mawazo Yako Yaweke kwa Huyu wa Sasa

Kwanza acha kumuwaza aliyepita. Mara zote jaribu kutafuta na kuona uzuri, utu na furaha ya kuwa na rafiki, mchumba au mwenzi wako wa sasa. Siku zote tafuta mazuri aliyokufanya au anayakufanyia huyu wa sasa na zingatia hayo.

2. Rejesha Mazuri ya Mwanzo kwa Kuyaboresha

Ikiwa kuna vitu, hali au matukio mazuri unayoyakumbuka kwa yule aliyekuacha, basi ni vema kujitahidi kutengeneza matukio kama yale hasa kwa yale yanayowezekana. Maana yake ni kwamba matukio mazuri uliyokuwa unayapenda kwa yule basi yasababishe yawepo na hapa. Najua si rahisi yakawa yote na wakati mwingine si rahisi sana kwa sababu ya utofauti wa watu ila nina uhakika rafiki yako wa sasa hatakuwwa na tofauti kubwa na wewe ikiwa hukukurupuka kuwa naye. Maana mara nyingi unawavutia watu unaofanana nao kitabia na hata kimtazamo. Like attract the like.

Ikiwa hukubadilika basi kuna uwezekano mkubwa wa rafiki yako wa sasa akawa na baadhi ya vijitabia vinavyofanana na yule aliyekuacha. Ndiyo! Na hivyo ndio vilikuvutia kwake kama vilivyokuvutia kwa yule aliyepita. Usishangae, tabia za huyu na yule aliyepita zinaweza zikawa tofauti saaaaana ikiwa ulikurupuka kuingia kwenye uhusiano kwa kutumia hisai- emotions au kwa sababu ya kuwa desparate. Na zinaweza zikawa tofauti saaana kama ulibadilika na kuchagua mfumo mpya wa maisha baada ya kuachwa au kuachana na yule wa mwanzo.

Mgahawani, Chakula, Vinywaji hata Maneno, Yaweza Kuwa Yaleyale

Kwa hiyo kama unakumbuka mgahawa mliokuwa mnaenda na yule wa mwanzo, basi unaweza kutafuta angalau siku moja mkaenda pale na huyu wa sasa. Ikiwezekana mnaweza kuagiza chakula kama kileeeee kama unakikumbuka au vinywaji hasa ikiwa inaweezekana. Maana kama ulikunywa pombe na sasa umeacha na inapaswa kuwa hivyo basi usinywe pombe. Unaweza kunywa kinywaji kikingine kisicho na kilevi. Hili si kwamba tu ni mtazamo wangu lakini pia nadhani nina uelewa unaostahili juu ya vilevi kwa mtazamo wa kisayansi, kisaikolojia na kiroho. Kwa hiyo si vema kutumia vilevi kwa nia ya kunywa kilevi. Wengine wataniuliza sasa iwe kwa nia gani? Najua si rahisi sana kunielewa na hili ni somo jingine tena pana sana, ila kwa sasa elewa hivyo. Usinywe kilevi kwa nia ya kunywa kilevi.

Ikiwa kuna maneno uliyoyazoea kumwambia yule wa mwanzo na ikiwa maneno hayo ni mazuri basi unaweza kuwa unamwambia huyu pia, yasiwe matusi au mtazamo hasi. Kama kuna aina ya nguo ulipenda sana kwa yuleee, basi unaweza kumshawishi na huyu na akavaa pia hasa kama ni nguo zinazojenga utu na si kumdhalilisha au kuabisha utu wa mtu. Kama ulipenda afuge ndevu, mwambie na huyu afuge, kama anazo za namna ile. Ndio maana nilikwambia si lazima kila kitu kifanane. Ila maadamu ulikubali kuwa na huyu na hana ndevu kama za yuleeee basi nina uhakika mkubwa kuwa ndevu inawezekana hazikuwa kigezo.

Sasa kama ulimwona yuleeee na kucha za bandia au macho ya dandia, namaanisha lenzi za macho za bandia, basi vumilia usimlazimishe na huyu aweke hizo za bandia.

Ikiwa ulibadilika au ulibadili mfumo wa maisha, basi kwa sehemu kubwa kutakuwa na vitu vingi vizuri kwa huyu wa sasa, ambavyo havifanani na yuleee, hasa kama ulirudi edeni. All in all, kumvulia nguo au kuvua nguo kwa rafiki au mchumba is forbidden, hairuhusiwi. Kanuni ni kwamba haijengi uhusiano ila inashusha utu na huharibu kanuni kadha wa kadha katika ulimwengu wa roho na hata wa mwili pia na matokeo yake ni maumivu ya moyo hata kama mtakuja kuoana. Kama mlijisahau mkadhani  mmekwishaoana, basi from now REPENT AND STOP!   UTUBU NA UACHE MARA MOJA. 

Kama anakuvulia nguo wewe usiye mumewe unadhani ni kitu gani kitamzuia asimvulie mwingine ambaye naye si mumewe? Au unadhani kama amekufanya wewe kama mkewe huku akijua hajakuoa unadhani nini kitamzuia asimfanye na mwingine? Fikiri tu polepole. Mtu makini aliye wa kweli anayeweza kujizuia asifanye ngono na wengine basi hakika ana uwezo wa kujizuia pia asikikuvue au kukuvulia nguo, mpaka hapo utaratibu wa edeni unapokamilika.

Okay, turudi kwenye valentine yetu. Siku zote pasipo na malengo hapawezi kuwa na nidhamu. Huwezi kuwa na nidhamu katika kila ufanyalo sasa kama huna malengo mahususi kwa ajili ya maisha yako ya sasa na ya baadaye. Ikiwa una malengo halafu ukakosa nidhamu basi upo kwenye mfumo mbovu wa maisha na hivyo unapaswa kubadilika mara moja kabla ya mauti kukufika. Ninajua mara nyingi ukiwa kwenye  mfumo mbovu unakuwa kama hujielewi elewi hivi, kama upo njia panda fulani. Japo wengine hubaki kulia na kuumia tu.

Badilika acha utoto, epuka kufuata mwili, usiongozwe na viungo vya uzazi, usiige tu mambo, ipo sababu ya wewe uumbwa na una thamani kubwa sana. Usiwe CHEAP hivyo bwana. Yaani kila mdada au mkaka akikutaka anakupata lo! Okay, sikulaumu ila nataka ufikirie vizuri halafu uishi maisha yako. Uache kuishi maisha ya watu. Ikiwezekana itakubidi kubadili marafiki ikiwa utaamua kuunganishwa Edeni kwa damu ya Yesu. Ukiona una dilema, huna uhakika kipi ni kipi, huoni sawasawa ubadilike au uache, fanya hivi:- Kaa chini tafakri maisha unayotaka kisha tafuta mtumishi unayemwamini na unayeona anaweza kukusaidia, hasa ukiwa na nia ya kuhitaji msaada kwa Mungu. Unaweza kuwasiliana nami kwa namba hizo hapo chini. Ni vema kuchukua hatua na kuunganishwa na aliyekuumaba, Mungu. Hii ni ili kukuweka katika mfumo aliounzisha yeye mwenyewe kwa kurejesha Edeni.

Nina mengi ya kukufundisha ila naomba niishie hapa hadi wakati ujao Ubarikiwe sana.

Dk George Adriano
Simu: +255 715 182 106
Tanzania

0 comments:

Post a Comment