Sunday, May 12, 2013

Akisaidia mtu mmoja Unaona kafanya kidogo.. Je angekusaidia wewe?

Habarini ndugu zangu. Natumai mu wazima kabisa. Mimi ni mzima ama baada ya salamu niwashukuru mnaoendelea kuchangia uchapaji wa kitabu chetu.. THE POWER OF CHOICE, mchakato unaendelea.

Wakati mchakato huu ukiendelea, nguvu ya kuandika bado ipo na inatiririka tu. niombe maombi yenu ili kila nitakachoandika kifanyike msaada kwa mtu fulani, hata kama ni mmoja. Unaweza kuona kama haina maana ikiwa vitachapwa vitabu nakala 1000 halafu kikamsaidia msomaji mmoja tu kati ya wasomaji 1000. Ila leo nimegundua kuwa kitu kinaweza kuwa na manufaa madogo au yasiwepo kama hakijakusaidia wewe, ila kama huyo mmoja kitakayesaidia kubadilika na kuwa na maisha mazuri utakuwa ni wewe bautaona umuhimu wa kitabu au kitu hicho.

Ninachotaka kusema ni kwamba hata kama unaona uwezo wako ni mdogo usidharau na kuona hufai maana hata ukiweza kumsaidia mmoja ni jambo jema sana, maana hujui huyo uliyemsaidia ataweza kuwasaidia wengine wangapi! ila kama sio msaada wako huenda sio tu akashindwa kuwasaidia wengine ila hata yeye angekuwa na hali mbaya.

Big up Mama maana kwa kunilea mimi umelea mamilioni watakaosoma vitabu vyangu kwa miaka mimgi ijayo.

Kitabu kipya BECOMING YOURSELF-SELF-REDISCOVERY AND REPOSITIONING hope kitakwa so powerful. Maisha yanaendelea


karibu
George Adriano

0 comments:

Post a Comment