Kwa sasa nimemaliza kuandika kitabu kitakachoitwa THE POWER OF CHOICE
nilichoanza kukiandika miaka miwili iliyopita. Vitabu vingine vilivyokamilika
ni UPENDO UPITAO UFAHAMU na BECOMING YOURSEL-Self-rediscovery and
Repositioning na kingine ninachoendelea kukifanyia kazi ni THE POWER OF LOVE
Baada ya kushauriana na watu mbalimbali nimeona ni vema
kuwashirikisha watu (wewe) katika uchapaji wa kitabu hiki na ukapata nakala ya
kitabu hicho.
HIvyo, ukiwa kama ndugu, jamaa, rafiki, mwanaharakati na
mpenda haki na maendeleo, ninaomba mchango wako wa hali na mali ili kufanikisha
uchapaji wa kitabu hicho cha THE POWER OF CHOICE.
Utaratibu huu wa mchango utafanana sana na tufanyavyo katika masuala ya arusi,
kitchen party n.k ila tofauti ni kwamba katika hili utapata nakala ya kitabu na
si chakula na vinywaji.
Mimi Dk George Adriano, nimejisikia kufanya hivyo si tu ili
kuchapisha kitabu lakini ni kwa sababu zifuatazo:
1.
Kushirikishana mawazo yetu kwa kusoma vitabu
2.
Kujenga utamaduni wa kusoma vitabu kama njia
mojawapo nzuri kujenga misingi ya maendeleo
3.
Kushirikiana katika masuala mengine ya msingi
kama tufanyavyo kwa suala la msingi la sherehe mbalimbali.
4.
Kuibua hamasa kwa vijana wa ki-tanzania na
wasomi kuandika vitabu
Mchango huu ni wa hiari, kila kitu kitakuwa wazi kwa kila
atakayehitaji matumizi na mchanganuo wake. Na pia nitajitahidi izekanavyo
kuhakikisha kila aliyechangia kazi hii anapata nakala ya kitabu bure, yaani
hanunui ila mchango wake utakuwa umetosha.
Asanteni sana, ikiwa una maoni au mchango wowote tafadhali
utume kwa namba zifuatazo:
Tigo Pesa: 0 715 182 106
M-Pesa: 0 767 182 106
Airtel Money: 0 786 182 106
Kupata
dondoo za kitabu tembelea page ya facebook. Bofya hapa chini
0 comments:
Post a Comment