Wednesday, March 13, 2013

Tutafika Kweli? Serious Naomba Maoni yako....!

Siku moja kila mtanzania atakuwa anajipatia mahitaji yake sehemu kama hii???????? Hebu nisaidie!!!!!!


Naendelea kutafakari kwa kina juu ya ushirikiano na umoja tulio nao watanzania katika masuala ya kijamii. Hii ni pamoja na Arusi, Sherehe ya Jikoni (Kitchen Party-Sina uhakika kama kweli ni ya jikoni au la), sherehe za ubarikio/kumunio na wakati mwingine hata sherehe za siku ya kuzaliwa (Birthday Party). Naelewa ushirika huu na sura hii ya upendo ambayo huwa tunaionesha ni nzuri, sherehe ikiisha kikubwa tunachokuwa tumefanikisha ni kwa wawili kuoana na kusherehekea na marafiki kwa uzuri na furaha ni jambo zuri. Baada ya hapo wengine tutaondoka na kushika hamsini zetu, tukiwa tumeshiba au hatujashiba, na wengine wakiwa wamelewa au hawajalewa.

Maisha yanaendelea. Natafakari, je  kuna uwezekano wa mtu au watu kufanya mchango wa aina iyo hiyo bila ya kukutana, kula na kunywa huku kukiwa na mziki na shamrashamra na badala yake unapewa kitu fulani? Mfano mimi ninataka kuprinti kitabu "THE POWER OF CHOICE" ninachotamani ni kwamba tushirikishane mawazo na namna mbalimbali za kuendesha maisha yetu kama wanadamu. Kwa hiyo badala ya mimi peke yangu kugharimia uchapishaji ila wewe/watu wakachangia na kisha ukapata nakala ya kitabu kikiishapwa na ukawa umesaidia mtu mwingine kuweza kununua nakala kwa bei nafuu na yeye akapata chochote kutoka kwenye kitabu hicho.

Mpaka sasa wengi wanaunga mkono wazo hili ila bado naendelea kuwashirikisha wadau na kuona namna ya kuiweka vizuri. Lengo langu si kupata faida kuuuubwa ila kushirikishana mawazo na kujengeana utamaduni wa kusoma na kuandika vitabu. Namshukuru Mungu kwamba sijapata maoni hasi (negative opinion) na wengine wameahidi kiasi cha fedha kabla hata sijaanza kuwatext.

Ndani ya moyo wangu napenda vijana tuwe na maono na malengo katika maisha. Kitabu kitakuwa kwa lugha ya Kiingereza. Nimeona ipo shida kidogo ya kimtazamo kwa vijana wengi na hata kwa walio vyuo vikuu au waliomaaliza vyuo vikuu. Ninatambua nguvu iliyopo kwa vijana tuliopata fursa ya kupata elimu ya juu. Ninaelewa mfumo wentu wa kiuchumi kwa kiasi fulani na namna inavyokuwa na ugumu wa kijana fresh form college/University kuwa absorbed na system. Tunahitaji kuwa na namna mbadala. Namna hii haianzii kwenye mazingira, ila ni lazima ianze katika fikra zetu kuwa na mtazamo mpya ili kutengeneza mazingira mapya. Ifike mahali badala ya vijana kulalamikia serikali au mfumo badala yake tunachukua hatua stahiki na kusababisha maboresho au mabadiliko tunayoyataka.

Hakuna mtu yeyote duniani anayeweza kukutengezea maisha yako (future). HAKUNA. Watu wengine wanaweza wakatenegeneza mazingira fulani ili wewe uyatumie kutengeneza maisha yako. Jukumu la kutengeneza maisha uako ni lako, si la mtu mwingine yeyote. Sasa ukielewa baadhi ya mambo kama haya utaelewa kuwa kama mfumo haukutengenezei mazingira mazuri hakuna maana kulalamika, ila ni kuchukua hatua ili kuyatengeneza mazingira, na wakati mwingine ikiwezekana unatengeneza mfumo utakoawazuia wanakuharibia mazingira ya kuendelea/kukua kiuchumi, kijamii n.k

Nisiendelee kuandika mengi, ila ninaomba mawazo yako, ushari, masahihisho yako na chochote unachodhani kitafaa ama kuboresha ninachofikiri na hata kukikosoa, KLaribu sana

Unaweza kunipigia 0715 182 106
George Adriano
Tanzania 

0 comments:

Post a Comment