Katika blog hii niliandika makala iliyokuwa na kichwa kinachosema 'Spika kulindwa dhidi ya wananchi tafsiri yake nini?" (Unaweza kuisoma hapa hapa www.adrianogeorge.blogspot.com)
Walichokifanya ni kumimina maji yote na kisha kuondoka. Maneno ya mkuu wa mkoa yamenifanya nifikirie mbali kidogo. Mh. Mahiza alisema, "Wiki iliyopita nusura nyumba yangu ichomwe moto... kwani maji yalikatika kwa wiki mbili hapa na wananchi kuamu kuvamia kwangu na kumimina maji yote niliyokuwa nimehifadhi kwa ajili ya mtumizi yangu" Akaendelea, "wananchi waliyumia nguvu na kujimiminia maji... sasa fikiria kama wasingekuta maji yaliyohifadhiwa nyumbani kwangu, ninaamini kabisa nyumba yangu wangeiteketeza kwa moto" Hii inanipa picha namna wananchi walivyokuwa na hasira. Sasa jiulize hasira juu ya mkuu wa mkoa au maji? Kumbe wao wanauwezo wa kuhifandhi maji ya ziada ndo maana hawatatui shida ya maji. Haya yaanaweza kuwa ndio mawazo ya wananchi kwa sasa. Tunakokwenda si kuzuri. Tunatakiwa kuwajibika.
Sio kwamba nashabikia maji kumiminwa ila najaribu kuunganisha kwa upana, uhusiano wa viongozi na wananchi wao. Mh. Spika Anne Makinda ameongezewa ulinzi na kubadilishiwa magari na namba za magari kwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari. Kwa huko mkoani Pwani, najiuliza kama tatizo la maji litaendelea hiyo mimina mimina ya maji itaendelea au yataongezeka mengine zaidi?
Kwa sasa utasikia mbunge kazomewa, mara mkuu wa mkoa amezomewa na wananchi. Mara naibu waziri akumbana na zomea zomea alipokuwa akihutubia. Tumesikia huko Mtwara, nyumba za wabunge kuchomwa moto na hata ofisi za CCM kuchomwa moto na wananchi.
Hawa ni watanzania waliokuwa wanajulikana kwa upole na ukarimu. Hii si dalili nzuri kwa watawala. Inaonesha uhusiano mbaya kati yao na wananchi. Swali linakuja je ulinzi utakuwa ukiongezwa kwa kila kiongozi badala ya kutatua changamoto zinazowakera wananchi? Kama hali itaendelea hivi je, kutakuwa na tofauti gani na utawala wa kidikteta? Japo wanaoelewa sifa za tawala za kidikteta na sifa za watawala madikteta unaweza kufanya compare and contrast.
Viongozi wajifunze kuwajibika pale wanaoshindwa au wanapotakiwa na wananchi wao kufanya hivyo. Kinyume na hapo wataiingiza nchi kwenye udikteta.
Wananchi ni wakati wa kusoma alama za nyakati. Nyakati za baadhi ya watawala wetu zimekwisha, tunasubiri muda tu ufike tufanye maamuzi. Hakuna haja ya kuogopa kuweka chama kingine madarakani. Kama kuna viongozi wazuri ndani ya Chama tawala na tunawajua tutawaambia wafanye nini ili tuwachague. Nao wanaakili. Kwa kuwa wana moyo wa kututmikia wananchi na kama moyo huo wataendelea kuwa nao, bila shaka watajiunga na wenzao wa chama kipya kuijenga nchi yetu inayoanguka au inayoangushwa na wachache.
Tafakari juu ya wajibu wako katika nchi yako, acha kulalamika, chukua hatua.
Dk George
Tanzania
0 comments:
Post a Comment