Saturday, March 15, 2014

TUMEAMUA KUHARIBU UWANJA WETU WA TAIFA?

Kwa muda sasa nimekuwa nikitafakari sana juu ya mambo yanayotokea Uwanja wa Taifa hapa Dar es Salaam. Utasikia uharibifu wa vifaa mbalimbali vya uwanja n.k. Washabiki na wapenzi wa mchezo wa mpira wa miguu (Soccer) ninahitaji mnijuze, mnijibu maswali yangu na mnifafanulie nini cha kufanya:

Hivi mtu anapovunja kiti, sababu hasa inakuwa ni nini? Je ni tatizo la akili au ni elimu duni na kukosekana kwa ustaarabu?

Mtu anapofungua koki ya maji au kuvunja sinki za vyoo vya uwanja wa taifa maana yake nini? Sababu hasa ni nini? 

Ni ulevi, ni ujinga, ni ukichaa, ni hasira, au ni nini. Unapovunja kiti au kuharibu kiti unataka kupeleka ujumbe gani kwa jamii? 

NImejaribu kufikiri nikiaishia njiani. Tunaona viwanja vikubwa duniani, tunaona timu kubwa hasa za nje washabiki wamejaa uwanjani wanashangilia kwa kuimba na hatuoni uharibifu wa viti kama hapa kwetu au viti vyetu ni vya kichina?

Naomba maoni yako:

1. Unafikiri sababu za mashabiki kufanya uharibifu katika uwanja ni zipi?
2. Unadhani nini kifanyike angalau kupunguza au kuzuia kabisa adha hii?
3. Wewe

huwa unajisikiaje, unaposikia au kushuhudia uharibifu wa aina hiyo?

Asante: Comment hapa, au African lives Dr. George Adriano face book page. 

0 comments:

Post a Comment